Posts

Showing posts from January, 2023

KITULO NATIONAL PARK MBEYA

Image
Hifadhi ya Taifa Kitulo ni hifadhi ya  Nyanda za juu Kusini mwa Tanzania katika mikoa ya Mbeya na Njombe. Hifadhi hii ipo kati ya kilele cha Milima ya Kipengere, Uporoto na  Safu za Milima ya Livingstone. Hifadhi ya Taifa ya Kitulo ina ukubwa wa kilomita za mraba  412.9.  Hii ni hifadhi ya kwanza kabisa barani Africa kuanzisha kwa lengo la kutunza mimea yake hususani jamii ya maua. Awali hifadhi hii ilijulikana kama “Elton Plateau” baada ya kugunduliwa na Fredrick Elton mwaka 1870. hifadhi ya Taifa ya Kitulo kuna aina mbalimbali za wanyama wakiwemo jamii mpya ya nyani aina ya kipunji, pundamilia na swala ambao waliletwa kutoka hifadhi ya taifa ya Mikumi. Vile vile kuna aina mbalimbali za vipepeo ambao husaidia kuchavusha maua,  vinyonga, mijusi na vyura. Pamoja na vivutio lukuki ambavyo  vinapatikana katika hifadhi hii, vile vile  kuna  uwanda wa tambarare, mabonde,vilima na maporomoko ya maji na mabwawa ambayo ni muhimu kwa ustawi wa mto Ruaha Mkuu ambao ni tegememezi kwa hifadhi ya T

ZIWA NGOSI

Image
  Ziwa Ngosi ni kreta kubwa ya pili Africa baada ya ile ya Ethiopia. Ngosi ina muonekano wa Bara la Africa ndio upekee wake linapatkana milima ya Upoloto Mbeya Tanzania. Ziwa hili limetokana na mlipuko wa volkano hivyo ni tofauti na maziwa mengine. Upekee wa ziwa hili ni kwamba liko ndani ya milima ya upoloto katikati ya misitu na lina urefu wa km 2.5, upana wake ni km 1.5, kina chake ni mita 74 na lina ukubwa wa hektari 9332. Maajabu mengine katika ziwa hili ni kwamba maji ya Ziwa Ngozi huwa lina muonekano wa rangi tofauti tofauti kila wakati, kuna wakati ukifika unakuta ziwa lina rangi ya samawati, kijani au nyeusi.  misitu husababisha rangi ya maji kubadilika. Ziwa hili halina wanyama hai wala halina hata samaki na wataalamu wanasema si salama kwa kuogelea. Karibu sana ziwa Ngosi karibu sana Mbeya. VisitMbeya Follow us through our twitter site @VisitMbeya

MBEYA PEAK/Kilele cha Mlima Mbeya

Image
  Kilele cha mlima Mbeya ni moja ya kivutio kikubwa sana kinachopatikana mkoa wa mbeya ambao uko nyanda za juu kusini. Ukiwa juu ya hicho kilele cha mlima unaweza kuona madhari nzuri sana ya huo mlima kuna ukijani mbichi sana wakati wa masi ka,kuna ndege wazuri sana pia kuna ardhi nzuri sana pembezoni mwa mlima ambayo ni nzuri sana kwaajili ya kilimo na wenyeji wa hayo maeneo kabila la wasafwa wanalima sana viazi mviringo/Ndokanya. Pia ukiwa kwenye kilele cha huo mlima unaweza kuona mbeya mjini kwa bondeni. Ni sehemu nzuri sana kwaajili ya kutembelea na ki refresh mind. Juu ya kilele hicho kuna upepo mzuri na baridi kiasi ambayo inaondoa joto kabisa. Karibuni sana Mbeya peak  Welcome and Visit Mbeya Tutafute kupitia twitter @Visitmbeya