KITULO NATIONAL PARK MBEYA
Hifadhi ya Taifa Kitulo ni hifadhi ya Nyanda za juu Kusini mwa Tanzania katika mikoa ya Mbeya na Njombe. Hifadhi hii ipo kati ya kilele cha Milima ya Kipengere, Uporoto na Safu za Milima ya Livingstone. Hifadhi ya Taifa ya Kitulo ina ukubwa wa kilomita za mraba 412.9.
Hii ni hifadhi ya kwanza kabisa barani Africa kuanzisha kwa lengo la kutunza mimea yake hususani jamii ya maua.
Awali hifadhi hii ilijulikana kama “Elton Plateau” baada ya kugunduliwa na Fredrick Elton mwaka 1870.
hifadhi ya Taifa ya Kitulo kuna aina mbalimbali za wanyama wakiwemo jamii mpya ya nyani aina ya kipunji, pundamilia na swala ambao waliletwa kutoka hifadhi ya taifa ya Mikumi. Vile vile kuna aina mbalimbali za vipepeo ambao husaidia kuchavusha maua, vinyonga, mijusi na vyura.
Pamoja na vivutio lukuki ambavyo vinapatikana katika hifadhi hii, vile vile kuna uwanda wa tambarare, mabonde,vilima na maporomoko ya maji na mabwawa ambayo ni muhimu kwa ustawi wa mto Ruaha Mkuu ambao ni tegememezi kwa hifadhi ya Taifa Ruaha.
Maporomoko haya ni kivutio kikubwa cha watalii wengi wanaofika hifadhi ya Kitulo hasa kwa utalii wa picha na mazingira “adventure tourism”.
Ukifika katika hifadhi ya taifa ya Kitulo unaweza kupata fursa ya kutembelea milima ya Livingstone ambayo ipo karibu na Ziwa Nyasa.
Karibu sana Hifadhi ya Kitulo Mbeya
Comments
Post a Comment